Ngoma Tano Zinazosikilizwa Zaidi Kwenye Smartphones!


Upo miongoni mwa wale wana watumiaji wa Android, Especially Tecno, Hope utakua sio mgeni wa kitu kinaitwa "Boom Player?".

Boom Player ni Application ambayo inakuja ikiwa installed kwenye Simu za Tecno, inamuwezesha mtumiaji wa simu kununua nyimbo za wanamuziki wa Afrika, Sambamba na kununua nyimbo, Mtumiaji wa Tecno anayo nafasi ya kusikiliza nyimbo alizohifadhi kwenye simu yake na zile ambazo zinauzwa kupitia App hiyo.

Kupitia streaming ya ngoma zinazouzwa Boom Player wanahesabu idadi ambayo ngoma imesikilizwa na kuzi-update charts zao, Kwenye Chart ya ngoma zinazotrend Afrika Mashariki Lady Jay Dee amesimama Namba 1 na ngoma yake " I Miss You" aliyoitambulisha rasmi Septemba 12,
Kutoka Kenya ni "Ndogo Ndogo" ya David Wonder na Bahati kwenye nafasi ya 2,

Walianza Kushirikishwa pamoja Kwenye "Monifere" ya Gosby, Wakaulizwa kama wana-date wakasema they're just working, wakashindwa kujizuia, wakaamua kuweka mapenzi yao wazi, Baadae Mapenzi kama  yakawa hayasomeki hivi, Mrembo Vee Money akajiwazia, "I got talent, Nasubiri nini?, let me write about this",
akaidropisha "kisela" ambayo ipo nafasi mbili za juu zaidi ya Utaniua Ya Ex- wake Jux ambae anashikilia nafasi ya 5 kwenye chati ya ngoma zinazotrend kwenye Application Ya "Boom Player" na bila  kusahau nafasi ya 4 imeshikiliwa na mwana mwingine kutoka Kenya ni Maluda na mkwaju wake "Nishampata"

#Kumbuka: Licha ya kuja moja Kwa moja kwenye simu za Tecno, App ya Boom Player inapatikana Playstore hivyo mtumiaji yeyote wa simu ya Android anaweza kui-install kwenye simu yake.

lilomy.com inazo ngoma 10 zinazosikilizwa zaidi mitaa ya DSM, Unachitakiwa Kufanya ni kudropisha Kura yako kuzidi kuipa mashavu ngoma unayoielewa au inayogongwa kinomanoma mtaani kwako kwa kuzama lilommy.com muda wowote.