Nandy alishindwa Kujizuia, Amwaga machozi LIVE kwenye Coke Studio Africa!

Betty G amtoa machozi Nandy kwenye Stage ya Coke Studio Africa baada ya kurudia wimbo wake wa One Day na kuumiza kinyama mbele yake, Nandy ambaye ni mshiriki kutoka Tanzania kwenye msimu huu wa tano wa Coke Studio Africa alishindwa kuzuia hisia zake na kumwaga machozi ya furaha baada ya Betty G wa Ethiopia alipokuwa akiimbia kwa hisia sana na kuupatia kinyama wimbo huo.

Haikuwa kwa Nandy tu, hadi mashabiki waliokuwepo ndani nao walipagwa, tazama hapa:Fuatilia show za Coke Studio Africa kwenye msimu huu mpya wa tano na uwezo kugundua vipaji vikali kutoka Afrika kwenye jukwaa moja, Ni Kila Siku za Jumamosi Saa 12 jioni CloudsTV.