Mr Nana "Giggy Money na Amber Lulu hawajui kuimba"

Msanii wa muziki kutoka visiwani Zanzibar Mr Nana amesema wasanii Giggy Money na Amber Lulu wanaimba nje ya key hivo hawana uwezo mzuri wa kuimba.

Mr Nana alisema hayo kwenye interview aliyofanya kwenye kipindi cha THE PLAYLIST Times FM Radio baada ya kuulizwa swali kwanini amewataja vibaya kwenye wimbo wake mpya 'Dar bila instagram' kwenye wimbo huo verse ya pili inaimba kuna timu Kiba, kuna timu Mondi mahodari kutukanana kwenye show hawaiingii,  album hawanunui, Kuna Amber Lulu Luna Giggy nasikia wameshika jiji, wanaimba nje ya key.

Mr Nana "Wanaimba nje ya key, unajua siku hizi mziki umekua katika instagram sana, kisa mtu ana followers instagram nae kesho asubuhi anaamka tu kawa msanii unashangaa"