Mimba Ya Kylie Jenner: Rappa Tyga Kaibuka Na Kauli Ya Kibabe


Oi niaje, kama kawa kama dawa, Ukisikia katajwa Jenner ujue ni drama mwanzo mwisho, Na hivyo ndivyo ilivyo, kama utakumbuka siku mbili zilizopita hapa lilommy.com tulikuletea stori ya Rapa Traviss Scott kumtia mimba mtoto wa moto model Kylie Jenner,

Sasa baada ya stori kwenda viral Rapa Tyga ameibuka na kudai kuwa mimba hiyo ni ya kwake, patamu hapo.

Kwenye Snapchat ya TMZ kuliwekwa stori ya Jenner na Traviss kutarajia mtoto wao wa kwanza mwezi Februari mwaka 2018, Baada ya Tyga kuisanukia post hiyo ali-share kwa Followers wake akiiongezea na Caption iliyosomeka "Hapana, Mtoto ni wangu" akiongezea na Emoji za kishetani,Kabla ya kutoka na Travis Scott, Kylie alikua kwenye mahusiano na Tyga yaliyodumu takribani miaka mitatu na walisharipotiwa kuachana mara kadhaa kabla ya kuachana rasmi mwezi April mwaka huu.

Kwenye Show yake "Life Of Kylie" mrembo huyo aliwahi kusimulia maisha ya mapenzi mpaka kuachana na Tyga, Alisema yeye na Tyga walikua vizuri changamoto za kwenye mapenzi zinatokea kwa kila mtu, Lakini ilifika pointi ilibidi waachane kwa amani kila mmoja afanye mambo yake.

Bata La Diamond Na Zari South Afrika, Kama Hakuna Stori Mbaya Kati Yao: