MANENO YA SHETTA BAADA YA KUPATA MTOTO

Shetta amepost picha Kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa amebeba kichanga huku akiandika maneno ya kumkaribisha mtoto huyo duniani.

"Karibu duniani mwanangu....!! Asante Mungu kwa huyu mwingine, sasa Kayla uache kuringa", ameandika Shetta.

Kufuatia kuzaliwa kwa mtoto huyo Shetta atakuwa na watoto wawili, ambapo wa kwanza anaitwa Kayla na mtoto huyu aliezaliwa amempa jina Qamrah.