Lady Jaydee: Mimi ni Shabiki wa Aslay

Malkia wa Muziki wa Bongo Fleva ambae anaweza kuwa ndio Msanii pekee wa kike Afrika Mashariki Lady Jaydee amesema yeye ni Shabiki wa Msanii @aslayisihaka ambae toka ameanza kufanya kazi kama Solo Artist ameshafikisha jumla ya Views Millioni 10 kwenye channel yake ya YouTube. Views hizo ni jumla ya kazi zake zote.

Lady Jaydee alieleza haya alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha THE PLAYLIST Times FM na LilOmmy wakati alipotakiwa kuchagua nyimbo 5 anazozipenda na moja wapo ilikuwa ni wimbo wa Aslay Muhudumu na kusema kuwa yeye ni shabiki wa muziki wa Msanii huyo na kwa sababu Aslay ana-melodies nzuri kwenye muziki wake.