Jana kupitia mitandao na blogs mbalimbali Bongo stori kubwa ilikua ni wimbo "Hallelujah" wa Mbongofleva Diamond Platnumz na Wajamaica "Morgan Heritage" ngoma ambayo imeivunja rekodi ya Youtube (Afrika) kwa kufikisha Views zaidi ya milioni 1 ndani ya masaa 15,
Kwa tafiti ndogo za haraka ikagundulika kama hapa Bongo kuna kizazi ambacho hakiwafahamu jamaa hao, Kwa msaada wa mtandao nimejaribu kukuelezea japo kwa ufupi kuhusu Kundi hilo.
Shuka Na Hii:
Shuka Na Hii:
Morgan Heritage ni kundi
la muziki wa Reggae ambalo mwaka 1994 liliundwa na Peter "Peetah"
Morgan, Una Morgan, Roy
"Gramps" Morgan, Nakhamyah
"Lukes" Morgan, na Memmalatel "Mr. Mojo" Morga, wote ni watoto
watano wa mkongwe wa muziki wa Reggae Denroy
Morgan.
Morgan Heritage wanamiliki Albamu zaidi
ya 10 ambazo zimefanikiwa kufanya vizuri kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20 ya
uhai wa kundi hilo.
Morgan Heritage kwa mara ya kwanza walionekana rasmi kama
kundi kwenye tamasha la Reggae Sunsplash pande za Jamaica,
Baadae wakalamba Deal ya kufanya kazi na MCA ( Music Corporation of America), Deal ambayo iliwapa nafasi ya kuiachia Albamu
yao ya kwanza “Miracles”
Baada ya kuaichia
Miracles, Memba 3 walijitoa kwenye kundi, Wawili waliobaki walianza kufanya
kazi na Bobby Dixon na Lloyd James ambao ni Reggae Producers wenye heshima
kubwa pande za Jamaica,
Albamu ya pili “Protect Us Jah” iliachiwa mwaka 1997,
ikifuatiwa na “One Calling” (1998), Mwaka uliofuta (1999) Morgan Heritage
waliachia “Don’t Haffi Dread kama Albamu yao ya 4 iliyofungua njia za Albamu nyingine
za Live zilizorekodiwa kwenye Tour zao za Uingereza na Ulaya,
Baada ya hapo
Morgan Heritage waliendelea kuachia ngoma moja baada ya nyingine mpaka 2013
walipoachia “Here Come the Kings”, Albamu iliyofuatiwa na Tour ya Ulaya.
Morgan
Heritage wameshafanya kazi na makundi na Madj kadhaa wa Reggae wakiwemo Capleton, Junior Kelly, Luciano, Gentleman na Beres Hammond.
Albamu ya “Strictly Roots”
iliyoachiwa 2015 ilishinda tuzo ya Grammy kwenye kipengele cha Albamu bora ya
Reggae mwaka 2016.
Unadhani Baada ya "Hallelujah" huenda Morgan Heritage watajikusanyia mashabiki wapya kutoka Bongo?
QuickRocka Amesema Diamond Platnumz Amevunja Rekodi: