Kutoka Kwenye "Lemonade" Ya Beyonce, Hii Ndio Ngoma Anayoikubali Michelle Obama

Mapema wiki hii aliyekua Firstlady wa zamani wa  Marekani Michelle Obama alipiga stori na watu kadhaa kwenye mkutano uliohusisha waandishi wa habari,

Kikubwa alichoongea Michelle ni kuhusu kitabu chake kitakachoelezea maisha yake ya Ikulu,mafanikio ya Mzee Barrack Obama, Nyakati alizopitia kuwalea wasichana wake Maria na Sasha Obama wakati taifa kubwa la Marekani likimuangalia kama mama mlezi kwa kipindi hicho.

Kwenye kipengele cha maswali na majibu Firstlady huyo wa zamani aliulizwa kuhusu ngoma anayoielewa kutoka kwenye Albamu "Lemonade" ya Malkia Beyonce, alianza kwa kujibu "zote" kwa vyovyote vile ilivyo, Lakini Love Drought ndio ngoma ninayoi-play muda mwingi", Lemonade ina ngoma zipatazo 12, "Love Drought" ndio ngoma anayoikubali mke wa Rais mstaafu wa Marekani, Tudondoshe Comment utuambie ngoma unayoikubali kutoka kwa Beyonce,

Angalia Jinsi P SQUARE Walivyozinguana, Mtiti Mzito!, Kundi Limeunjika: