Picha Za Petitman Na Hamisa Zimevuja, Petitman Kafunguka Anachokijua.


Instagram Bongo imekua Bonge la uwanja kiasi kila kitu kinapatikana huko, Asubuhi ya leo Septemba 26 picha zinazowaonyesha model Hamisa Mobetto akiwa kwenye mkao matata na Pettitman Wakuache zimeanza kusambaa kwa kasi ya 4G.


Pages mbalimbali za udaku zime-share picha hiyo kila moja kwa mtazamo wake,Baada ya stori ku-trend Petitman ameibuka na kufunguka anachokijua kuhusu picha hizo, Kwenye ukurasa wake wa Instagram Petit amepost picha yake na babymama wake Esma huku akiongezea jinsi anavyomkubali,


"Picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii ni za zamani sana. Hazina uhusiano wowote na maisha yangu ya sasa au na yale yanayoendelea kuhusu Hamisa ambaye anaonekana pia katika picha hizo kwa sasa. 

Yeyote ambaye ameamua kuzisambaza ana nia moja tu. Kuniunganisha katika suala ambalo sihusiki na kunichafua. Mimi kwa muda mrefu niko na mke wangu mpendwa ambaye kila mtu anamjua na tuko busy kujenga familia yetu. Inawezekana jambo hili haliwafurahishi baadhi ya watu hivyo kuamua kusambaza picha za zamani kwa nia zao ovu. 


Niseme tu kwa kifupi hizo picha sio za kutilia maanani. Ni picha za zamani sana. Kwa sasa sio muda wa kuchafuana. Huu ni muda wa kila mmoja wetu kupambana kujijenga na kulea familia yake. Mimi kama baba wa familia jukumu langu ndio hilo." ameandika Petitman WakuacheTUJIKUMBUSHE:
Petitman amemuoa Esma ambae ni Dada wa Diamond Platnumz, Kama Petitman Aliwahi kum-date Hamisa maana amechangia mwanamke na Shemeji yake ambae upande wa pili aliwahi kuwa Baba yake kwa Wema Sepetu (Natania), nadhani ukifuatilia vizuri zaidi hilo cheni unaweza kupata sisi wote ni ndugu, Noma sana,Bata La Diamond Na Zari South Afrika, Kama Hakuna Stori Mbaya Kati Yao: