Hamisa Mobetto amtunishia Zari ‘Waambie waliopanga mwenye nyumba kaja’

Acha movie iendelee. Hamisa Mobetto jamani ni shida – azidi kumtia presha Zari The Bosslady.


Wiki hii Hamisa, Zari na Diamond wameteka vichwa vya habari mpaka nje ya nchi, hasa baada ya baba wa mtoto kufahamika. Vita iliyopo sasa hivi ni kuhusu malkia halali ambaye ataimiliki ikulu ya Madale.


Hamisa ameonyesha kutupa mawe gizani kupitia mtandao wa Snapchat na yameonekana kumfika mlengwa wake ambaye ni Zarina Hasssan (mama Tiffah). Kubwa zaidi ambalo limewashangaza wengi ni ujumbe alioandika wa kutamani kuzaa watoto mapacha na kujinadi kuwa yeye ndio mama mwenye nyumba.
Haya ndio aliyoyaandika Mobetto kwenye mtandao huo.
Source:Bongo5

TAZAMA INTERVIEW YA Hamisa Mobetto Na Diamond Platnumz.


HAMISA MOBETTO Kwenye THE PLAYLIST