DROGBA MWAFRIKA MWENYE MAGOLI MENGI ZAIDI LIGI KUU YA UINGEREZA.


Wachezaji wa kiafrika waliowahi kucheza ligi kuu ya uingereza na kuacha historia kubwa ya ufungaji magoli, wapo wengi, ila Didier Drogba ndiye aliyeweza kufunga magoli mengi zaidi kwa wakati wote. Amefunga magoli 104 akiwa na Chelsea Fc.

 DIDIER DROGBA (CHELSEA)Ni legend pale darajani, ni mfalme pale Ivory Coast, ni miongoni mwa wachezaji ambao Afrika kwa ujumla tutaendelea kujivunia waliwahi kucheza ligi kuu ya uingereza, Drogba aliletwa Uingereza na kocha Jose Mourinho mwaka 2004, akitokea klabu ya ufaransa Marseille kwa dau la Paundi 24 Millioni. Tokea kipindi hiko amekuwa mchezaji tegemeo pale chelsea na aliwapa taji hilo mara 4, misimu ya 2004/05, 2005/06, 2009/10, 2014,15.