Diddy amewabuluza Drake, Jay-Z, Birdman kwa kuwa na Mkwanja Mwingi ZaidiDiddy ameongoza list ya Wasanii wa Hip Hop Marekani wanaolipwa mkwanja mwingi zaidi 'Highest Paid Hip Hop Artists' kwa mwaka 2017 ingawa hajaachia Album yoyote ile sokono.

List hiyo iliyotolewa na Forbes ikiwa na wakali wa Hip Hop 20 wenye kisu kirefu zaidi duniani, walimtaja Sean Combs Diddy aka Puff Daddy aka P Diddy kama Msanii wa Hip Hop ambaye amelipwa mkwanja mwingi zaidi kwa mwaka 2017 na kukadiriwa kiasi cha $130 Million kutoka katika michogno mbalimbali.

Diddy ametajwa kushika nafasi hiyo na kuwabuliza wakali kibao kutokana na michongo Channel yake ya Televison, RevoltTV, Kinywaji chake chake cha Ciroc Vodka, DeLeon tequila na maji yake ya Aquahydrate water. Pia kuna deal alipiga la kuuza kidogo sehemu ya brand yake ya mavazi 'Sean Jean Clothing Compay na kupiga kama $70 Million hivi. Diddy alisema "I've always understood that if I give the customers my best and service them differently, whether music, clothing or vodka, I'll get a return on my hard work," aliichana forbes.

Utakumbuka kuwa Diddy hajatoa Albumu yoyote mwaka huu zaidi ya kupiga tour na show ya pamoja na member na wasanii wake wa zamani wa Bad Boy Records na alifanya muunganiko wa miaka 20 ya Bad Boy Entertainment. So kama kungekua na Album huenda mwanja ungekuwa mrefu zaidi ya mkwanja alioingia nao wa $130 Million.

Aliyefuta katika list ni Drizzy Drake amesogea namba 2 kwa kiasi cha $94 million kutokana na Tour yake ya Boy Meets, mauzo ya albumu zake Views, More Life na deal alilopata na Apple na Srint pamoja na deal la Nike.

Jay-Z amedondoka katika nafasi ya 3 na mkwanja wa kiasi cha $42 million. kaika list kuna wakali wengine kibao lakini Msanii pekee wa kike katika list hiyo ni Nick Minaj na msanii mpya aliyezama na wakali hao ni Lil Yachty akiwa na $11.5 million.


katika picha Kushot ni Jay-Z, Katikati ni P Diddy na kulia ni Drake.

Diddy amekuwa anabuluza kwenye list za forbes kwa miaka 7 sasa mfululizo kwa kuongoza nafasi ya kwanza.

1. Diddy - $130 million - (Billioni 291.8)
2. Drake - $94 million - (Billioni 211)
3. JAY Z - $42 million - (Billioni 94.2)
4. Dr. Dre - $34.5 million (Billioni 77.4)
5. Chance the Rapper - $33 million - (Billioni 74)
6. Kendrick Lamar - $30 million - (Billioni 67.3)
7. Wiz Khalifa - $28 million - (62.8)
8. Pitbull - $27 million - (60.5)
9. DJ Khaled - $24 million - (Billioni 53.8)
10. Future - $23 million - (51.6)
11. Kanye West - $22 million
12. Birdman - $20 million
13. J. Cole - $19 million
14. Swizz Beatz - $17 million
15. Snoop Dogg - $16.5 million
16. Nicki Minaj - $16 million
17. Lil Wayne - $15.5 million
18. Macklemore & Ryan Lewis - $11.5 million (tie)
19. Rick Ross - $11.5 million (tie)
20. Lil Yachty - $11 million


YOUNG D ' Dogo Janja na Young Killer ni Vifaranga Vyangu, Hawawezi kufanya Show na mimi'