Diamond amtumia Ujumbe huu Zari kwenye birthday yake, Sifa za moto moto kibao


Sept 23 ni Siku ya kuzaliwa ya The Bosslady Zari, sasa baada ya Diamond kukitibua kwa Zari na kukiri kuwa mtoto wa Hamisa Mobeto ni wake siku chache zilizopita, Chibu ameenda kwenye page yake ya Instagram usiku wa Sept 23 mida ya Saa 6 na nusu usiku na kuwai kabla hakujakucha ili awe mtu wa kwanza kumtakia birthday Zari, ujumbe wake ulikuwa umejaa Sifa kibao kwa Zari ambaz alizimwaga wazi wazi kuonesha kuwa Zari ndio chaguo lake.

Diamond alinadika hivi kwenye page yake. Uzuri na Urembo pengine ningetembea nikakuta baadhi wanao pia... Lakini Akili, Hekma, pamoja na Roho yako ya kwenye Shida na Raha kwangu ndio kitu pekee kinachonifanya nikupende na kukuthamini zaidi kadri siku zinavyozidi kwenda...... wanaposema kwenye kila Mafanikio ya Mwanaume kuna Mwanamke imara nyuma, hawamaanishi eti anaepika na kuosha vyombo sana ama kufua nguo kila siku... Hapana! ni mwanamke Mwenyekuwa bega kwa bega na Mpenzie kwenye Shida na Raha... Happy birthday General­čĺ×


YOUNG D ' Dogo Janja na Young Killer ni Vifaranga Vyangu, Hawawezi kufanya Show na mimi'