CHEGE 'Sijawahi kulipia COLLABO YOYOTE TOKA Nimeanza MUZIKI, Kuna Msanii alitaka nimlipe nikamtosa'

Chege Times FM kwenye The Playlist

Msanii wa Bongo Fleva Chegge Chigunda mtoto wa Mama Saidi amesema hajawahi kulipia Collabo yoyote ile toka ameanza muziki, Chege aliongeza kuwa kuna msanii aliataka alipwe kufanya Collabo kwenye ngoma yake ya Counter ya Juu ila alimchomolea na kuwashirikisha Mandojo na Domokaya.

Chege alisema pia ela nyingi ambayo walipata wakati wapo kama kundi Manyema Family ilikuwa ni Tsh laki mbili na elfu hamsini (250,000/=) na pesa hiyo walilipwa na Dj JD ambaye aliutumia wimbo huo kwenye mixtape yake.

Chege Times FM kwenye The Playlist

Chege alichana exclusive kibao kwenye interview aliyofanya Times FM katika kipindi cha The Playlist na Lil Ommy.

Tazama full VIDEO hapa chini.