BEN POL:SAWA SOKO LA ALBAM KWELI LIMEYUMBA LAKINI TUTAFANYAJEMkali wa rnb BONGO Ben Pol ameachia albamu yake ya THE BEST OF BEN POL licha ya kuonekana kuwa kwa Bongo soko la albamu bado linayumba.

Albumu ina nyimbo 15 na ndani yake kuna wakali kama Mr Eazi wa Ghana, Darassa, Linah, Rama Dee na Chidinma wa Nigeria.


Alisema Ben Pol kwenye interview aliyofanya kwenye kipindi cha The Playlist, Times FM 'Soko la albamu la nyimbo za wasanii BONGO limeonekana kuwa hakuna mauzo mazuri endapo albamu ikiingia sokoni, lakini hivi sasa baadhi ya wasanii wameamua kutoa albamu zao licha ya kujua kuwa sokoni hakuna mauzo mazuri ''kweli albamu sokoni biashara hakuna lakini tutafanyaje.? 

Je tukae kimya kwamba tusifanye au tufanye ili kuinspire watu wengine wafanye ili baadae tutakuja kutafuta ufumbuzi kwa pamoja'.

Albamu ya Ben Pol imeshatoka na inapatikana kwenye itunes, Spotify, Youtube, Apple Music, Tidal, Amazon Music na Google Play, Pia albamu hiyo ya THE BEST OF BEN POL kuna Collabo za kibabe alizofanya na mkali Mr Eazi wa Nigeria, Darasa, Rama D, Chidinma wa Nigeria na Linah.

Ben Pol amewaomba mashabiki wa muziki wa BONGO FLEVA kusupport muziki wa nyumbani na wawe tayari kununua albamu ata kama wakiusikia wimbo kwenye radio, ameongeza mkali BEN POL

UNAWEZA UKACHECK  BEN POL AKIHOJIWA KWENYE SHOW LA KIBABE THE PLAYLIST BONYEZA HAPA KUITAZAMA