Barnaba atangaza ujio wa albamu yake Mpya 8/8 yenye ngoma kumi

Msanii wa Bongo Fleva Barnaba Classic ametangaza kuachia albamu yake ndani ya mwaka huu.


Akipiga stori katika The Playlist ya Times Fm, mkali huyo  amesema kuwa baada ya  kushindikana kuachia albamu  hiyo hapo mwanzoni kutokana na matatizo aliyopata ila sasa ana mpango wa kuachia albamu hiyo yenye ngoma kumi hivi karibuni.
“Mimi ni muimbaji nimetamani kuiona albamu yangu ikienda sokoni, i wish watu wasikie albamu yangu ambayo inakuja hivi karibuni,” amesma msanii huyo baada ya kusikiliza nyimbo zake mbili ‘Tunafanana’ na ‘Loverboy’ na kuongeza kuwa “baada ya kuzikiliza nyimbo hizi mbili naona yani kama zimebeba nyimbo 100 ukiachia zile nane zilizo bakia.”

Pia msanii huyo akasisitiza kuwa jina la albamu yake  itaiwa ‘Eight eight’ (8/8) sawa na siku yake aliyozaliwa na akaeleza kuwa  alipanga itoke albamu hii siku nyingi ila kutokana na matatizo aliyopata ya kuibiwa ikacheleweshwa hivyo kwa sasa  wana kaa na menejimenti kupanga mipango mizuri zaidi ya kuitoa.

Pia aliongeza kuwa katika album hiyo, barnaba amesema kutakuwa na wimbo aliofanya na Maua Sama na watautoa na Video kabisa. Aliongeza kuwa ukiachia mbali yeye, Dee Classic, Tuddy Thomas album hiyo itashirikisha producers wa Kenya, South Africa kuongeza ladha na vionjo tofauti.