Baada Ya Kwenda Platinum Mara 2, @KendrickLamar Ametangza UK & EUROPE "DAMN" Tour


D A M  N ni Albamu ya nne ya rapa Mmarekani Kendrick Lamar iliyodropioshwa rasmi April 14 mwaka huu, Albamu ambayo ilipokelewa kwa kasi ya 4G na walio na wasio mashabiki wa Kendrick Lamar, kwani wiki Yake ya mwanzo tu D A M N ilifanikiwa kuishika Namba 1 kwenye chati za US Billboard 200 ikiwa ni Albamu ya 3 kutoka kwa Kendrick Lamar kupata chance ya kuwa Number 1 Album Marekani na namba 2 kwenye UK Albums Chart.

Mastaa wakubwa duniani walimpongeza Kendrick baada ya kurelease Albamu hiyo, 

D A M N  pia ilipata nafasi ya kuchukua tuzo sita za VMA kupitia ngoma ya H U M B L E peke yake.

 Forbes kwenye list ya Wanamuziki wa Hip Hop walioingiza Mkwanja mrefu mwaka huu wamemtaja pia Kendrick Lamar hiyo yote ni kutokana na mauzo mazuri ya D A M N.

Kampuni ya RIAA ambayo hufuatilia mapokeo na mzunguko wa Singles na Albums iliitangaza DAMN Kuwa Double Platinum Certified,

Miezi miwili baada ya kwenda Platinum mara mbili, Kendrick Lamar ametangaza Tour ya Albamu hiyo Ulaya na Uingereza,


D A M N ina jumla ya ngoma 14, zilizopata nafasi ya kutangazwa zaidi ni Humble, DNA na Loyalty aliyoshirikishwa Badgirl Riri, Ipi Ngoma unayoikubali kutoka kwenye Albamu hiyo?


JAYMOE 'Siwezi kununua VIEWERS ingawa namba zina maana sana' WE ALL NEED NUMBERS Now: