ASLAY 'MIMI NI SHABIKI MKUBWA SANA WA BEKA FLAVOUR'


Msanii anayefanya poa kichizi kwenye Bongo Fleva time hii, Aslay na ngoma zake kibao alizotoa Back to Back na vyupa bila kusikilizia muda mrefu amesema kuwa yeye ni Shabiki mkubwa sana wa Msanii Beka Flavour.

ASLAY alishuka kwenye kipindi cha The Playlist Times FM kuchangua ngoma 5 anazozikubali na ngoma ya kwanza kuichagua ilikuwa Libebe ya Beka Flavour na Lil Ommy (Mtangazaji) alitaka kujua kwanini kachagua wimbo huo?

Aslay 'Ngoma ya kwanza ni ya ndugu yangu Bakari Beka Flavour inaitwa Libebe, Mi kwanza ni mshabiki wake mkubwa toka tupo kwenye bendi halafu cha pili melodies alizoimba humu na vitu navyokumbuka kwenye bendi naona mwanangu anazidi kunishawishi kuwa shabiki wa milele na milele'

Tazama interview ya Aslay kwenye THE PLAYLIST Times FM.