Another One: DJ Khaleed Na P Diddy Kwenye Hip Hop Deal Ya Pamoja


Ukipewa mtihani wa kuwataja watu muhimu kwenye game ya HiP Hop/Rap ya Marekani huenda ukafeli Vibaya zaidi usipowataja Puff Daddy na Dj Khaled,

Jarida la Forbes ambalo hutoa ripoti  muhimu za watu maarufu kila mwaka, lilimtaja Diddy kama mwanamuziki wa Hip Hop anaemiliki mkwanja mrefu zaidi kipindi cha miezi sita ya mwisho wa mwaka jana mpaka sasa,

Kitendo cha kuwachukua wanamuziki wengi na kuwachanganya kwenye ngoma ya pamoja kimeendelea kujenga heshima ya jina la Dj Khaled, Licha ya kufanikiwa vizuri kwa projects zake, Dj Khaled ndiye staa anayekik kwenye mtandao wa "Snapchat"

Hold on, Ishu haikua kukuambia nani ni nani na anafanya nini, Ishu kubwa ni tetesi za wawili hao kusaini deal ya  kuonekana kwenye TV Show itakayokwenda kwa jina la "The Four", Show ambayo itakusanya wakali wanne kutoka kwenye Industry ya Hip Hop, wakigawana majukumu kama Producers na Judges, Zoezi ni kutafuta star mpya wa Hip Hop ambae atapata nafasi ya kufanya kazi na mastaa hao.

Taarifa rasmi kutoka kwa wawili hao bado hazijawekwa wazi mpaka muda huu, Hii inakua mara ya pili kwa Dj Khaled kutajwa kuhost show kubwa nyingine mwaka huu baada ya kutajwa ku-host Usiku wa Tuzo za "BET Hip Hop" kwa mara ya pili mfululizo baada ya zile za mwaka jana.Angalia Jinsi P SQUARE walivyozinguana, mtiti mzito!, Kundi Lavunjika: