Angalia Hapa Balaa La Young Thug Kwenye Birthday Ya Demu Wake Jumatatu ya Septemba 18 mrembo Jerrika alisherehekea siku yake ya kuzaliwa na kwa mujibu wa post yake kwenye mtandao wa Instagram,  Rappa Young Thug alitoa zawadi ya gari aina ya Range Rover kama zawadi kwa mrembo huyo kutimiza umri wa miaka 24.
Young Thug kupitia ukurasa wake wa twitter alimpongeza mrembo wake kwa kuzielezea hisia zake na jinsi anavyomkubali mpenzi wake huyo, kwa kuandika  "Happy birthday to the love of my life, one of the best girls in the world to me,".

Haikuchukua round mrembo Jerrika kuuona ujumbe huo muhimu kwake kwani dakika chache baadae aliujibu kwa kuandika "Thank you soo much for making all of my birthday special, I Love you foreverrrrrrrrr"

Young Thug kwenye moja ya Inteview zake aliwahi kutangaza ujio wa Albamu itakayokua ikimuhusu mrembo Jerrika, "You Guys should look out for this Album," "I'm making a whole Album about her, It's gonna be Perfect, lakini licha ya kuitangza kwa muda mrefu Albamu hiyo Young Thug hajawahi kutoa tamko rasmi kuhusu ujio wala kuonyesha Cover na Idadi ya ngoma zitakazosomeka kwenye Albamu hiyo,

Kwenye Interview hiyo hiyo mrembo Jerrika alipata fursa ya kuongea kuhusu maisha ya mahusiano yake na Young Thug, kwa kumpamba kuwa mshikaji ni zaidi ya mwanaume linapokuja suala la kumtuliza mtoto mzuri, "Ananifaa, Naweza kusema ni mwanaume wa maisha yangu, Nampenda, anajua mwanamke anahitaji nini ili penzi liendelee kustawi" alisema mrembo Jerrika,

Sio mara ya kwanza kwa Young Thug kutoa Gari ya gharama kama zawadi kwa watu wake anaowakubali, July mwaka jana Young Thug aliripotiwa kuwanunulia Magari na nyumba zake za kuishi kaka na dada zake 12.