ALIKIBA, VANESSA NA DIAMOND WAIBEBA TANZANIA KWENYE TUZO HIZI

Wasanii Ali Kiba, Vannessa Mdee pamoja na Diamond Platnumz wamechaguliwa kuwania katika tuzo za Middle East Africa Music Award (MEAMA)

Tuzo hizo ambazo zimepangwa kufanyika tarehe 5 Oktoba mwaka huu, zina lengo la kuibua vipaji na kuonyesha hamasa kwa wasanii wa Afrika kwa ujumla.

Wasanii kutoka mataifa makubwa ya Afrika kama Kenya, Uganda, Nigeria, Sudan Kusini, Tanzania, Misri na mengineyo watashiriki.

Kwa upande wa Tanzania msanii wa kike Vannesa Mdee ndiye msanii pekee wa kike kutoka Tanzania aliyewekwa katika kategori ya msanii bora wa kike wa mwaka, huku akichuana na Victoria Kimani, Yemi Alade na Seyi Shayi.

Kwa upande wa wanaume, Ali Kiba amewekwa katika kategori ya msanii bora wa kiume wa mwaka, huku hasimu wake Diamond Platinumz akigombea kategori ya wimbo bora wa mwaka (Eneka)

Wasanii wengine wanaoshiriki kuwania Tuzo hizo kutoka nchi tofauti na Tanzania ni pamoja na Davido, Wizkid, na Mr.Eazi.

Zoezi la upigaji kura limeanza jana Septemba 13, huku mwisho wa kupiga kura ikiwa ni Septemba 30 mwaka huu. Hafla ya ugawaji tuzo imepangwa kufanyika kufanyika Oktoba 5 nchini Misri.

Credit: infoHD