ALIKIBA AMETOA SOMO LA JINSI YA KUACHIA NGOMA MPYA, PASIPO KUKURUPUKA.

Mwanamuziki wa bongo fleva Alikiba, akiwa kwenye interview ya thePlaylist ametoa soma la jinsi ya kutoa wimbo mpya, kwa kusema kuwa muziki kwake ni kama bidhaa na hawezi kutoa wimbo mpya mpaka pale utakapoisha sokoni.
Image result for Alikiba

King kiba alisema pia, kwa kiasi kikubwa yeye anawasikiliza zaidi mashabiki zake, wakianza kuhitaji na kulalamika mtandaoni na sehemu nyingine ndipo hupata wazo la kutoa wimbo mpya, kwa ajili ya kuzuia malalmiko kwani muda mwingine, anaogopa kama wanataka kumpiga vile.

Related image

"Kuna muda inabidi uache wimbo ufanye vizuri kidogo, unapoona umeshindwa kupumua ndio unatoa mwingine" - ALIKIBA

Ila kwenye Seduce Me Alikiba alisema anasubiri ukifikisha 10 Million views kwenye Vevo (Youtube) ndipo atakapo toa wimbo mpya.

Hivyo ndivyo Alikiba anavyotoa nyimbo zake, na hiyo ndio sababu ya yeye kukaa muda mwingi pasipo kutoa ngoma mpya.