Drake Amefikisha Tattoo 30, Baada Ya Rihanna Na Lil Wayne Angalia Hizi Mpya Alizoongeza


Inal Bersekov ni mshikaji mmoja hivi maarufu kwa uchoraji wa Tattoo pande za Ubeligiji, Kwenye Instagram page yake mwana ametupia picha zinazoonyesha Tattoo mbili mpya ambazo amemchora mnyamwezi Champagnepapi (Drake) moja ikiwa ni ya Fif, moja kati ya watu ambao wamekua sehemu ya maisha ya Drake lakini kwa bahati mbaya mshikaji alifariki wiki iliyopita kwa kupigwa Risasi pande za Toronto, Canada.

 Mbali na ushikaji  pia Fif alikuwa ni “Labelmate” wa Drake kwenye chama la “Ovo Sound”, Drake kwenye instagram page yake aliandika juu ya kilichomkuta mshikaji  kwa kupost picha sawa na ile ambayo Inal Bersekov alitumia kuonyesha Tatto alizomchora rappa huyo.
 


Akiwa Ontario, Canada Inal Bersekov amesema ni heshima kupata fursa ya kuchora tatto hiyo kwenye mwili wa Drake “Honored to pay tribute tattooing “FIF” on my brother Drake.” Aliandika kwenye page yake ikiwa na picha yenye tatto ya (Fif) mshikaji wake Drake aliyefariki,
Tatto nyingine ambayo  staa huyo wa “More Life” amechora wiki hii ni sura ya Muigizaji Danzel Washington, Kuhusu hiyo Bersekov (Mchoraji Tattoo) ameandika “Mo’ better blues” first seassion on my brother (Drake), Thanks as usual  for your trust.” Clarke: ‘Cause mo better makes it mo better” huku akimtag @DanzelWashington1.
Kwa mujibu wa source za karibu na Drake, kwa sasa Mcanada huyo amefikisha tattoo 30 kwenye mwili wake zikiwemo sura za watu miongoni mwao ni Baba yake mzazi, Lil Wayne, Marehemu Aaliyah na zilipendwa wake Rihanna.