AliKiba: Wasanii Wa Zamani Walikua Wanapendana, Siku Hizi Watu Wanalewa Usupastaa,

Wote tunafahamu kama Alikiba ndiye mwanamuziki aliyekaa kwenye midomo na vichwa vya habari mbalimbali Bongo na nje ya mipaka ya nchi za jirani kama Kenya.

Alikiba  amekua gumzo mjini baada ya kuachia "Seduce Me" ngoma ambayo imekua na mapokezi chanya kutoka kwa mashabiki na wadau wa muziki wa Bongoflava.


 
Kwenye mahojiano yake na #ThePlayList" ya Times FM, Alikiba amefungukia kinachoonyesha kuitesa game ya bongoflava kwa kile alichokitaja ni Chuki baina ya wasanii...

"Natamani wasanii wa sasa wajue vile ambavyo wasanii zamani walikua Wanapendana, Maisha ya kiusanii yamechukua nafasi kubwa, usupastaa unawapoteza watu wana-act maisha. Alisema Alikiba.

Kwenye sentensi nyingine Kiba amesema Unaweza kuwa na pesa na nafasi kubwa ila fahamu kama hakuna mwenye pesa kama pesa ni yako iweke ndani uone kama utasurvive,

"Kila mtu ajiangalie ndani ya nafsi yake, Sisi ni wamoja, Tusiabudu maisha ya ustaa yatutawale, Tuwe na Umoja.

MSIKILIZE HAPA ZAIDI: