B.O.B Haamini Kama Dunia Ni Duara, Anachofikiria Kufanya Ili Kuthibitisha Hilo


Mwanamuziki wa Marekani rapa B.o.B. anatafuta msaada wa kutuma satelaiti kuthibitisha iwapo kweli dunia ni duara.

Rapa huyo ambaye jina lake halisi ni Bobby Ray Simmons Jr, ni mmojawapo ya watu wanaoamini kwamba dunia ni kama sahani na sio duara, Kwani kama ingekua duara kutokana na mzunguko wake basi vitu vyote vingekua vikianguka kutokana na kushindwa kukaa sehemu moja.
Anajaribu kuchangisha Dola 200,000 kwenye mtandao wa kuchangisha mkwanja wa GoFundMe na mpaka sasa amefanikiwa kukusanya kiasi cha Dola 650, lakin kampeni hiyo imekuwa ikizungumziwa kwa mapana katika mtadao huo.

"Nimeanzisha kampeni hii kwasababu ningependa kutuma kama sio satelaiti moja basi nyingi katika anga za juu kujaribu kutafuta upinde unaoifanya dunia kuwa duara," alisema katika video iliowekwa kwenye mtandao huo.


JIONGEZE! Utafanyaje ili USIKOSEE Kutuma PESA kwa mtu unayetaka zimfikie na zisiende kungine: