Wakazi: Chidi Benz Zima Kiki Washa Muziki


Miongoni mwa ishu zinazotikisa kwenye ulingo wa Bongoflava wiki hii ni uwepo wa ngoma mbili zinazosumbua mjini ambazo ni Seduce Me ya Alikiba na Zilipendwa ya Diamond Platnumz akiwa ameshirikiana na vijana wake wa WCB Wasafi. Katika KUPERUZI kwenye mitandao leo nimekutana na post ya Rapa Wakazi ambae ameonekana kumuunga mkono rapa mwenzake Chidi Benz ambae kwa muda sasa skendo ya utumizi wa madawa ya kulevya imekua ikimuharibia jina mpaka muonekano wake.

"Hiyo clip ya Chidi Beenz mbona wengine moja kwa moja mmeanza kumjaji ?! Issue ya Unga inatoka wapi?! Kama alichoongea mnahisi ni that disturbing basi mtafutieni msaada kwanza kabla ya kumhukumu. Lazima tuweke mezani all possible options kabla ya kupitisha moja kwa moja judgement, tena ambayo our course of actions after it ni kutikisha kichwa na kusema "Dah" au "Maskini Chidi" badala ya kumkwapua from that condition.
 
Yes inawezekana alichoongea ni ishara ya mental instability, ila hakina tofauti na Dayna Nyange kusema "Drake ni shemeji yake", au Young Dee kusema "Atachukua RB kwa mtu aliyevujisha Picha zake za Uchi alizopiga mwenyewe kwa hiari". Je kama Chidi ameamua kutafuta Kiki kwa kufanya kitu outrageous and divert the attention from SeduceMe/Zilipendwa By Ali Kiba & Diamond ?! That's the name of the Game right?! Kiki alafu unafata muziki au sio?! And by the way, hip hop community ya marekani huwa yote inasemaga "Tupac is in Cuba" sio Eminem sio Kendrick Lamar!! A drug addict is a patient, so is a Mentally unstable person. The former can birth the latter. Chidi zima Kiki Washa muziki, maana muziki unauweza haswa!! Ila kama hii ni an indirect cry for help, I'm urging everyone to do just that. © BEBERU"  

Ameandika Wakazi Kwenye ukurasa wake wa Instagram katika picha inayomuonyesha Chid Benz akifanya mahojiano na moja ya kituo cha TV alichokiambia kuhusu mipango yake ya kurudi rasmi kwenye muziki ikiwemo Collabo na Marehemu 2PAC, Kauli ambayo imeonekana kupokelewa kwa mtazamo hasi. 

  Kwenye kauli nyingine Chidi Benz amewataka mashabiki kutosikiliza maneno ya wapinzani wake ambao wamekua wakitumia nguvu kubwa kuzisambaza habari zake mbaya kila zainapotokea.