Muungano Wa Nicki Minaj Na Quavo Unaweza Usimuache Mtu Salama


 Nicki Minaj kupitia ukurasa wake wa Instagram ameshea na mashabiki wake kile kinaitwa ni teaser ya video yake mpya na memba wa kundi la Migos, QuavoHuncho

Kwenye Clip anasikika Nicki akiipamba ngoma hiyo kuwa moja ya mikwaju ya hatari ambayo mashabiki wake hawajawahi kusikia halafu mnyamwezi Quavo anapigilia msumari wa moto kwa kusema sio siri tena.Kwenye tetesi za chini kwa chini Nicki Minaj anasemekana kuwa busy na uandaaji wa Albamu (Taarifa zisizo rasmi) hivyo huenda ngoma hiyo na Quavo ikaja na kitu cha ziada.