MSIMU MPYA WA KIPINDI CHA THE PLAYLIST TIMES FM WAZINDULIWA KIBABE!


Show kubwa ya Burudani kwa vijana Bongo kwenye Radio ya THE PLAYLIST inayoendeshwa na Mtangazaji mkali mwenye uwezo mkubwa wa kuhoji mastaa na kuuliza maswali ya akili yenye details na ujanja mwingi, Omary Tambwe aka Lil Ommy inayoruka kupitia 100.5 Times FM Dar es Salaam, Tanzania ilizindua Msimu wake Mpya wa Jumatatu hadi Ijumaa na kualika mastaa kiboa na baadhi ya mashaki wa kipinchi hicho ndani ya Studio za Times FM na kufanya Party ya ufunguzi wa Kipindi, Kukata keki, kuchoma nyama na kunywa vinywaji kibao kitu ambacho ni cha historia kufanyika kwenye Media Bongo.


Msimu huo ulizinduliwa Agosti 7, 2017 Siku ya Jumatatu katika Lounge na Garden ya Times FM huku kikiwa LIVE On Air na kipindi kilikuwa na burudani zaidi huku Lil Ommy alikua akitoa historia kwa kufipi ya kipindi kilivoanza, mafanikio yake na sura mpya ya kipindi kwa sasa ambapo show hiyo inaruka siku za Jumatatu hadi Ijumaa, Saa 8 mchana hadi Saa 12 jioni tofauti na zamani ilikuwa Jumapili, ikaja Jumamosi na sasa ni siku za kazi (weekdays).


Lil Ommy, alielezea kuna vipengele vimeongezeka kwenye show hiyo kukiwa na sehemu INBOX uwanja wa vijana kutuma maoni yao, pia kuna sehemu ya kupata habari za burudani (INDUSTRY BUZZ), JIONGEZESehemu ya kupata maujanja ya mjini na kuwa macho usiingie chaka na zingine.Kipengele cha Mastaa kuja kuchangua ngoma 5 wanazozikubali kipo palepale ambapo kwa sasa wanakuja mastaa wengi zaidi kwenye show kuliko zamani ilikuwa mara moja tu kwa wiki na zaidi kumekua na Dj J One na Mtangazaji mungine wa Kike, Kattie wameongezeka kwenye show.

THE PLAYLIST Ni Kila Jumatatu hadi Ijumaa, Saa 8 hadi Saa 12 jioni kupitia 100.5 Times FM na Mnyamwezi Lil Ommy.

Picha:

    Lil Ommy - Host wa Show ya THE PLAYLIST
     DJ J ONE - DJ wa THE PLAYLIST Tahiya, Producer Dupy na Dj Choka
Tahiya na Angel Mary kato

 

 Lil Ommy - Brand Manager na Host wa show.
 Kattieeh - Co host wa show ya The Playlist K Hood na Lil Ommy na Jygga Lo

 Almasi Mzambele na Lil Ommy
 Shabiki - anajiita Harmonize Official fan

 MCB Quan na Lil Ommy
 Aaliyah  na Lil Ommy
 Nickmills na kattieeh
 Allen Donald - Producer wa kipindi na Lil Ommy

 Maggie Vampire na Lil Ommy Ben Temidayo wa Social Media na Lil Ommy


ASANTE SANA Wadau wote waliofanikisha na kusponsor uzinduzi huu, Jack Daniels, Diamond Karanga, Mak Juice Sinza, Coca cola na Keinos BBQ.

SHOW LA KIBABE THE PLAYLIST Kila Jumatatu hadi Ijumaa na Mnyamwezi Lil Ommy, Tambweeeeeee kupitia 100.5 Times FM.Unyama ule ule.