Kanye West Na Kim Kardashian Wanatarajia Mtoto Wa Tatu Januari HiiStori ya rappa Kanye West na mke wake Kim Kardashian kutaka kuongeza mtoto wa tatu kutoka kwa mama mwingine ni moja kati ya zile stori zilizobeba vichwa vya habri kwenye blogs na Media nyingi za Burudani mapema mwezi Juni mwaka huu.

Kwa mujibu wa US Weekly  Kim Kardashian anaripotiwa kuwa na tatizo kwenye mfumo wake wa uzazi hali iliyomsababishia kushindwa kushika mimba ili amzalie Kanye mtoto mwingine, 
Kilichofanyika ni kumtafuta mwanamke ambae angeweza kupandikizwa mimba ili azae mtoto atakaeifanya idadi ya watoto wa wanandoa hao kufikia watatu.

Habari njema ni kuwa mwanamke mwenye ujauzito wa miezi 3 tayari ameshajitokeza kuchangamkia deal hiyo ambayo malipo yatakua ni dola 45,000 za kimarekani sawa na milioni 10.7 za kibongo (Kila mwezi) kwa miezi kumi hivyo mjamzito huyo atakua amejivunia mkwanja wa zaidi ya milioni 170 za Kibongo.

Kim na Kanye pia wameahidi kumlipa dalali aliyefanikisha zoezi hilo mkwanja unaofikia Dola za kimarekani  68,850 zaidi ya milioni 154 za kibongo.