@JohMakini: Baada Ya #KataLeta Na @Iam_Davido Mashabiki Wasubiri Mkwaju Mkubwa Zaidi

Mwanamuziki Joh Makini anaeunda familia ya kundi la Weusi amesema anachopigania kwa sasa ni kufanya kazi bora zaidi zitakazoweza kumtangaza kimataifa.

Joh Makini ambae kwa takribani mwezi mmoja sasa anmekua akitamba na "Kata Leta" ngoma ambayo amemshirikisha Mnigeria Davido amepiga stori na Mtanzania kuweka wazi baadhi ya mipango aliyonayo ambayo itamsaidia kwenda mbele zaidi.

"Sio wasanii wa Bongo tu, hata nje sasa hivi muziki umekua na ushindani mkubwa, Mipango yangu ni kuachia ngoma kali ili kwenda sawa na soko la sasa" Amesema Joh Makini.

Joh Makini amekaririwa kwenye sentensi nyingine akisema "Nimegundua ili ufanikiwe ni lazima uvuke mipaka utafute watu wa nje  wanaofanya vizuri ili kushirikiana nao, Baada ya Kata leta na Davido mashabiki wasubiri ujio wa kazi nyingine kubwa zaidi" Alimaliza Joh Makini.


Joh Makini Ft Davido - Kata Leta (Official Music Video)