Fresh Ya FidQ Inapowafanya DiamondPlatnumz na Rayvanny Kugeukia Game Ya Hip Hop

Agosti 13 ambayo ni siku yake ya kuzaliwa rapa mwenye vina na mashairi ya kuumiza kichwa Fareed Kubanda "FidQ" alidropisha ngoma mbili kama ilivyo kawaida yake kuachia ngoma mpya kila baada ya mwaka mmoja.

Fresh ambayo ni moja ya ngoma hizo imeonekana kuwa na mashabiki wengi zaidi mmoja wao akiwa ni Mbongofleva Diamond Platnumz ambae kwa mujibu wa verse yake kwenye remix ya ngoma hii anaonekana kuikubali ngoma hiyo tangu siku ilipoachiwa, 

Kwenye moja ya line zake Diamond amesikika akisema "Nilipousikia mti tu nikatamani nifanye verse, nikamcheki Ngosha akaniambia Simba mbona fresh, Upesi Upesi nikaandika mistari ni-murder-e kesi na sas hivi ngoma mtaani imenuka kama kinyesi". 

Diamond ameitumia "Fresh Remix" kuwachana haters, mdomo wake na mtoto wa Hamisa,

Na thegood thing ni kwamba sio Diamond uliyemzoea, kuna Diamond Rapa alongside Tiddy Hotter's Beat iliyofanywa mixing na Magic Finger Laizer Classic.

Fareed Kubanda "FidQ" ambae ndie masterermind wa game hiyo hajacheza mbali na kile alichokifanya kwenye Original Version.

Vee  Van Boy ameumiza kwenye Chorus na kuikamilisha Rasmi Remix hii:

Cheki Nayo Hapa: