Alichokikuta Tanzania Kimemsahwishi Bilionea Bill Gates Kujiunga Instagram
Mkurugenzi wa Kampuni  ya Microsoft na Bilionea namba moja duniani Bill Gates yupo nchini Tanzania ambapo ana ziara ya kutembelea miradi na jamii mbalimbalimbali.

Tofauti na watu wengine maarufu, Bilionea huyo hakuwa miongoni mwa matajiri wanaotumia mtandao wa Instagram, Akiwa wilayani Muheza, Tanga Tanzania Bill Gates amefungua ukurasa wake rasmi kwa jina la “thisisbillgates” na kushea picha iliyomuonyesha akipata Chakula na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kicheba,
Habari Instagram, Kutokea Tanzania,

Nilikuwa na chakula cha mchana watoto katika Shule ya Msingi ya Kicheba huko Muheza na nilikutana na Upendo Mwingira, daktari wa ajabu ambaye amejitolea kazi yake kupambana na magonjwa ya kitropiki yaliyopuuzwa.

Melinda na mimi tumekuja Tanzania kwa miaka mingi sasa. Siku zote ninapenda kuona jinsi maendeleo ambayo nchi imefanya kuboresha afya na kutoa fursa. pamoja na mazingira ni ya kuvutia.

Wakati wowote ninaposafiri kwenye maeneo kama hayo, napenda wengine waweze kuja na kukutana na watu ninaowasiliana nao.

Sina shaka bila kuwaacha kuwa matarajio kama mimi ni miongoni mwa wale wanaotaka maendeleo yatokee duniani kote.

Nitakua nikishea picha zangu na nyinyi kupiti ukurasa huu na nina imani mtaungana na mimi.
Ameandika Bill Gates kwenye picha zake alizopost kwa mara ya kwanza kwenye mtandao huo unaotajwa kufikia wastani wa watumiaji milioni 700 kwa mwezi.

Kwa mujibu wa Forbes Bill Gates anatajwa kuwa na  utajiri wa Dola bilioni 89.5 za kimarekani ukiachana na zile dola bilioni 31.1 zilizopo kwenye taasisi yake ya “Gates Foundation.”