Chance The Rapper Ameikamilisha Orodha Ya Fortune "40 Under 40", Ndie Mwenye Umri Mdogo ZaidiAkiwa na umri wa miaka 24 tu Chance The Rapper ameikamilisha orodha ya Fortune “40 Under 40” akitajwa kama ndiye mwenye umri mdogo zaidi, Orodha hiyo imewataja vijana 40 wenye ushawishi kwenye biashara duniani.

Mikataba yake na Brands kama Apple,Nestle na Nike ni miongoni mwa vigezo ambavyo Fortune wamevitumia kumpa Chance nafasi hiyo, Kingine kinachoonekana kuwa kivutio zaidi kwa mshikaji huyo kuingizwa kwenye list ni ushindi wake kwenye Tuzo 3 za Grammy mwaka jana 2016.

Licha ya kufurahiwa na jamii ya Chicago mji ambao anatokea Chance ni miongoni mwa Rapa wakali ambao Rais mstaafu wa Marekani Barrack Obama anawakubali kinomanoma.

Mbali na Chance The Rappervijana wengine 39 walioikamilisha Orodha hiyo ni Mgunduzi na Mmiliki wa Facebook Marc Zuckerberg Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Mcheza Tenisi Serena Williams na wengine unaweza kuwacheki hapa.