Wafahamu Waliofanikisha Kuirekodi Albamu Mpya Ya Wizkid


Starboy Wizkid alidropisha Albamu yake "Sound From The Other Side" mwishoni mwa wiki iliyopita, Albamu hiyo yenye jumla ya ngoma nane imesheheni kila kitu ambacho mashabiki wa Wiz wanapenda kuvisikia kutoka kwa mkali wao.
 

Kinachoonekana kuwa kivutio zaidi ni mchanganyiko wa waandaaji walioshiriki katika kuikamilisha albamu hiyo. Major Lazer, DJ Mustard na DJ Maphorisa ni miongoni mwa waandaaji (Maprodyuza) waliokamilisha #SFTOS.
Come Closer aliyomshirikisha Drake, African Bad Gyal Ft. Chris Brown, Sexy na Sweet Love zimetengenezwa na SARZ. Moja kati ya Wanazmuziki/Producers wakali Nigeria, Licha ya kutengeneza hits kibao za Wizkid ameshawahi kufanya kazi na Banky W, Wande Coal, Skales, Reminisce, Marehemu Goldie Harvey na wengine wengi.
 


Licha tu ya  kuingiza fleva zake kwenye Daddy Yo, Dre Skull amabae ni producer kutokea New York ametajwa kuwa na mchango mkubwa katika kuikamilisha Albamu hiyo.

Kama ulikua hujui chochote kuhusu "Naughty Ride" Ft Major Lazer taarifa ikufikie kuwa Major Lazer ndio wamehusika kwenye mdundo huo.


"Dirty Wine" ambayo Wizkid ameshirikiana na Ty Dolla $ign imetengenezwa na DJ Mustard. Producer anaesifika sana Pande za Los Angels Marekani kwa mchango wake kwenye game ya Hip Hop na R&B.

Kutokea South Africa mwanadada Bucie amepata shavu la kuwa mwanamuziki pekee wa Afrika aliepata kolabo kwenye Albamu hiyo na ngoma "All For Love" iliyosukwa na DJ Maphorisa ambae tayari ameshasuka midundo ya wanamuziki wengi wakali wakiwemo Drake, Black Coffee, Uhuru na wengine wengi.
Trey Songz na Wizkid wameungana  kwenye ngoma GBese iliyorekodiwa na Producer Del'B aliyetengeneza hitsong "Limpompo" ya KCEE, amekua akitajwa miongoni mwa producers wakali Nigeria.

UNAWEZA KUISIKILIZA HAPA ALBAMU NZIMA: