Dr. Dre Kuingia Studio Na J. Cole, Ngoma Mpya Na Albamu Ya EminemKinachoonekana kuwa kivutio zaidi kwenye game ya hihop pande za Unyamwezini Wikiendi iliyopitai ni matukio ya wasanii tofauti kuonekana maeneo ya studio wakijaribu kutengeneza kazi za maana zaidi ili kwenda sawa na upepo wa industry vile unaenda race, Yaani ukilala wanaku-overtake...

Prodyuza Dem Jointz ambae  amefanya hits kadhaa za DRE amepost picha inayowaonyesha Dr. Dre washikaji wengine watatu pamoja na J. Cole wakiwa studio huku maandishi (Caption) ikisomeka "Blue Lights" ishara kwamba huo mwanga wa blue ulikua na sababu ya kuwashwa muda ule wa usiku, Asilimia 100 tunaamini kuna hitsong ya baade ilitengenezwa usiku huo.


A post shared by Dem Jointz (@demjointz) on


Licha ya kuwa na ngoma mpya "Gunfiyah", Kuna tetesi kuwa Dre anatengeneza albamu ya tisa ya rapa Eminem, Huku stori nyingine inayoonekana kusambaa kwa kasi ya 4G ni kuhusu  rapa J. Cole kuonekana studio baada ya ukimya mrefu.