Baada Ya Ku-shine Na Drake Wizkid Aungana Na Rapa HuyuHaiwezi kuwa rahisi akaja mtu kupingana na ukweli kama WizKid yupo kwenye level za mbali kwa sasa kufuatia hatua anazoendelea kufikia kwenye muziki wake,

 Ilianza kama masihara tukamsikia kwenye One Dance na Drake mara African Bad Girl na Breezy, Muda umepita tangu Wizkid aanze kushika headlines kwenye mitandao mikubwa ya iburudani zikiwemo XXLMag, The Fader na mingine mingi kitu ambacho kimemuongezea Credit kibao Mnijeria huyo.

 Wizkid ambae anajipanga kuiachia Album yake "Sound From The Other Side" Julai 14, amewathibitishia mashabiki wake kuwa ameongezwa kama "SPECIAL GUEST"  kwenye msafara wa ziara ya rapa mmarekani FUTURE  "The Future HNDRXXX Tour" ambayo itaanza mapema mwezi huu mpaka Oktoba mwaka huu.Mbali na kuhudhuria ziara hiyo huenda "Sounds From The Other Side" ikaja na ngoma ya pamoja na FUTURE kwa mujibu wa picha ambayo Wizkid aliwahi kupost kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwaonyesha wawili hao wakiwa pamoja.