Ushindi Wa Rayvanny BET Ni Funzo Kwake Na Wabongofleva Wengine


Tuzo Za #BET2017 zilifanyika June 25 Pande za Los Angeles Marekani huku zikimuacha na ushindi kwenye kipengele cha New International Act. ( Viewers Choice). Mbongofleva Rayvanny.

Haikuwa furaha kwa Rayvanny peke yake kwani nyomi liloungana na timu nzima ya WCB kumpokea  Uwanja Wa Ndege Wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere lilitosha kuthibitisha furaha ya wabongo kufuatia historia aliyoiandika Rayvanny ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda Tuzo hiyo.

BET ni tuzo kubwa zinazotambulika  dunia nzima zikiwashirikisha wasanii wakubwa wa kimataifa, Bila shaka wafuatiliaji wengi wa tuzo hizi kutoka sehemu tofauti Duniani watakua wameanza kumfuatilia Rayvanny ili kumjua zaidi. bahati nzuri kijana wetu hajawahi kuvuruga tangu alipotangazwa kama msanii wa Pili kusainiwa na Wasafi Record kisha kutamba na hitsongs "Kwetu" baadae "Natafuta Kiki" na sasa "Zezeta"

Wakati Bongo tukiendelea kufurahia ushindi huo imani yangu inanituma kuwa Rayvanny ana kibarua cha kuendelea kutengeneza ngoma ambazo zitaishi na kufanikiwa kupenya kimataifa zaidi ili kuitetea tuzo yake badala ya kuridhika na Tuzo moja tu, Itakua ni furaha ya ajabu tukiendelea kuona Rayvanny na Wabongofleva wengine wakizidi kutajwa na kuzinyakua tuzo tofauti za kimataifa.

Mwisho kabisa ningependa kuungana na wabongo wengine waliofurahishwa na ushindi huo kumtakia Rayvanny safari njema yenye mafanikio makubwa kwenye muziki wake. Wasanii wengine pia mnayo nafasi kubwa sana ya kutisha kama Mbeya Boy, Wabongo wanaelewa mnachokifanya msiwaangushe kwa kutoa 2days hit.