Luludiva: Sijawahi Kumilikiwa Na Serengeti Boy, Bill Zangu Nalipa Mwenyewe

Ubuyu unaoenea kwa kasi ya kiherehere unamhusu hitmaker wa  "Usimwache" Lulu Abbas "Lulu Diva" anaedaiwa kutoka kimapenzi na Kiserengeti boy.
Kwa mujibu wa gazeti la Ijumaa inasemekana Lulu amekua akijitenga na marafiki zake kuficha aibu ya kuhudumiwa mambo mengi na kiserengetiboi chake.

"Sijui anafanya kazi gani lakini ndiye anayempa Jeuri kuanzia Muziki mpaka mjengo anaoishi" Chanzo kililiambia Gazeti Hilo.

Gazeti hilo lilipomtafuta ili kujibu tuhuma hizo Luludiva alikanusha na kudai kuwa hajawahi kumilikiwa na kiserengetiboi na kama ni gharama na bills zote hujilipia mwenyewe.