Rayvanny Na Jason Derulo Watengeneza Historia Kenya


Kama kawaida Coke Studio Africa imerudi na kama tulivyozoea wanamuziki na maprodyuza mbalimbali wa Afrika  na mwanamuziki mmoja kutoka Unyamwezini wanapata fursa ya kukutana  kipande cha Nairobi Kenya zinapigwa Mash-Up kama zote huku msimu ukimaliza kwa makolabo mengi ya kimataifa.

Jason Derulo amedondoka +254 kwa kazi moja  nayo ni kukamilisha msimu huu wa mwaka 2017. Mtanzania Rayvanny ni moja ya wanamuziki wa kwanza kupata chance ya kuperfom kwenye stage moja na Jason Derulo,

 

Sahau Kidogo Kuhusu BET Rayvanny Anataka Uone Hii;Jason Derulo X Ray Vanny Live Performance Nairobi
Wakati Rayvanny yuko Kenya muda huo zoezi la upigaji kura wa Tuzo Za BET 2017 unaendelea na zali limemdondokea pia kwa kutajwa kwenye kipengele cha Msanii Mpya Wa Kimataifa, Rayvanny hayuko peke yake anashindanishwa na Jorja Smith (Uingereza), Dave,(Uingereza), Amanda Black (South Africa), Changmo (Korea), Daniel Caesar (Canada), Remi Kolawole (Australia) na Skip Marley (Jamaica)

  Mimi na wewe tunaombwa kuhakikisha Tuzo hii inakuja nyumbani Tanzania kwa kumpigia kura mara nyingi tuwezavyo. Nenda kwenye page za  BET chafua kurasa zote kwa ku-weka Hashtag #iPickRayvanny.