Nas Anakuja Na Kitu Fresh Kwa Ajili Yako, Sanuka Na Hii Ujue AnachokifanyaNasir Bin Olu Dara Jones maarufu kama Nas amekuepo Duniani tangu Septemba 14, 1973, Tangu kujihusisha kwake na harakati za muziki mwishoni mwa miaka ya 80 rapa huyu raia wa marekani anatajwa kuwa na Album zaidi ya 10 ambazo zimewahi kufanya vizuri duniani kote.

Kama utakua ni mfuatiliaji wa muziki wa mbele basi huenda ulikutana na hii Kolabo ya  Dj Khaled ft. Nas - Nas Album Done, Lakini hiyo haikutosha kukuthibitishia kama Nas yuko mbioni kuamsha dude lingine kwa mwaka uliopita (2016).

DJ Khaled - Nas Album Done ft. Nas


Ni zaidi ya miezi sita sasa tangu kolabo hiyo kuwepo kwenye platform tofauti za muziki lakini hakuna dalili ya ujio wa Album kutoka kwa Nas,

Kwenye Interview yake na NY Times Nas amekubali kuongelea kinachoendelea kwa sasa, Kitu ambacho hakutaka kukiweka wazi kipindi cha nyuma.

 “I always say I’m two weeks away from finishing, We coming this summer, baby!” Amesema Nas alipokua akijibu swali kama amefanikiwa kumaliza Albamu hiyo ambayo imekua ikisubiriwa kwa muda mrefu sasa.