Kufuatia Ujio Wa Mapacha Wao JAY-Z Na Beyonce Watatumia Zaidi Ya Milioni 800 Kulipia Nyumba Kila Mwezi


Beyonce na JAY-Z wameripotiwa kuwatoa watoto wao mapcha hospitali walikozaliwa na kuwapeleka nyumbani, Kwa mujibu wa TMZ couple hiyo inadaiwa kupanga mjengo wenye vyumba kumi vya kulala na eneo kubwa linalowatosha kujiachia bila kubugudhiwa kivyovyote vile unaolipwa dola 400,000 (Sawa na  894,800,000/= za kitanzania) kwa mwezi.

Chanzo cha karibu na fmilia hiyo kimeiambia TMZ kuwa familia nzima ya The Carter yaani Jay, Beyonce na watoto wao watatu watahamia kwenye nyumba hiyo mpya mpaka watakapopata nyumba ya kudumu pande za Los Angels,

Sio tu mapacha ambao Beyonce atajivunia kuwapata mwezi huu ushindi wa vipengele 7 ikiwemo Msanii Bora wa Kike na Album Bora (Lemonade) kwenye Tuzo za BET zilizofanyika Wikiendi iliyopita ni kitu kingine Beyonce anajivunia.