Kingine Kipya Kutoka Kwa Davido Na Wizkid


Takribani wiki mbili zimepita tangu Davido amedropisha hitsong "Fall" ambayo kwenye moja ya Lines zake amemtaja mwanasoka wa kimataifa Cristiano Ronaldo ambae baadae Davido kupitia ukurasa wake wa Instagram alipost picha yenye maelezo kuwa Cristiano Ronaldo amemfollow.Hasimu wake mkubwa Wizkid ambae yupo kenye hatua za mwisho za utengenezaji wa albamu yake "Sound From The Other Side" alipost picha akiwa na mnyamwezi Future,

 Sasa Jana kwenye ukurasa wake wa twitter Wizkid ameandika maneno ambayo yalisomeka.. "The FUTURE you see is better than the Footballer you don't"


Unaambiwa baada ya kukutana  na hiyo tweet Davido ali-reply povu lililosemeka 
"The footballer that follows you and don't see, is bettter than the DRAKE that never come closer". Akiwa na maana bora yake yeye ambae hajakutana na Ronaldo lakini anamfollow kuliko Wizkid ambae Drake ni mshikaji wake lakini hajawahi kuonekana kwenye ngoma zao za pamoja.

Davido na Wizkid ni wanamuziki wanaoipeperusha vyema Afrika kwenye industry ya muziki lakini Licha ya wote kutokea Nigeria washikaji hao wanaishi kwenye Beef ambayo imedumu kwa muda mrefu sasa.