Jokate Mwegelo Na Rosa Ree Kuuwasha Moto Muda Wowote Kuanzia SasaUkiwataja wadada wanaofanya poa kwenye Industry ya urembo hauwezi ukalisahau jina la Jokate Mwegelo, Anafahamika kama mshindi wa pili wa shindano la Miss Tanzania mwaka 2006 ambapo mwanadada Wema Sepetu aliibuka kama mshindi kwenye kinyang'anyiro hicho, Mbali na urembo Jokate amekua akijihusisha na uimbaji, Ngoma kama King and Queens Ya AY, Kaka Na Dada Ft. Lucci ziliwahi kututhibitishia kama Jokate ana uwezo mzurimkwenye suala la uimbaji.

 Ni muda mrefu umepita sasa bila ya Jokate kusikika kwenye ngoma mpya tangu tulipomsikia mwanzoni mwa mwaka 2014 alipoiachia Leo Leo ambayo rapa Mnaijeria Ice Prince Zamani alipewa mashavu.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya Kijamii Boss huyo wa brand ya "Kidoti" amevunja ukimya kwa kutangaza ujio wa ngoma yake na rapa wa kike anaekuja kwa kasi zote nchini Rosa Ree.


Ooh My God, Tunalijua balaa la Rosa Ree right?, Hebu piga picha sauti za hawa warembo kwenye mdundo wa pamoja, Haifichiki kama itakua ni hit.. Okay tuyape muda masikio yetu tukiwa tunaendelea kusubiri ujio wa kolabo hiyo ambayo haijawekwa wazi ni lini itaanza kupatikana.