Harmonize Kafunguka Kilichompeleka Marekani, Sio Mpenzi Wake

Msanii wa Bongo Fleva kutoka lebo ya WCB, #Harmonize amesema safari yake ya Miami nchini Marekani ilikuwa ni kwa ajili ya kazi na sio kupumzika, huku akitoa sababu za mpenzi wake ‘Sarah’ kujumuika nae.

Kwa mujibu Wa @bongo5  Harmonize  amesema si kweli kwamba alienda kutambulishwa nyumbani kwa mpenzi wake kwani walishafanya hivyo siku nyingi. “Miami nilikuwa na project sio kupumzika, kuna vitu nilikuwa nafanya, nina project kubwa sana Mwenyenzi Mungu amebariki imeisha salama na nimerudi, nilipokuwa kule wife alikuwa na project zake,” “Yeye pia alikuja kule kwa sababu sasa hivi Italy kuna baridi sana, kwa hiyo Miami ni mji kama una joto kidogo. Sio utambulisho mbona siku nyingi tushatambulishana. Halafu pia alitakiwa asafiri hapa katikati kwa sababu kitoto kikishakua kikubwa atazuiwa kupanda ndege, sasa hivi ale good time asafiri, asafiri kidogo,” alimaliza @Harmonize_tz

Staa Huyo Wa ngoma #ShowMe aliingia Kwenye headlines  baada Ya kutemana na staa Wa #BongoMovie #JackleenWolpe na kuzama Kwenye penzi  na #Sarah mrembo mwenye asili Ya Kizungu.