Dj Khaled ameendelea kusumbua kwa ujio wa Album yake mpya GRATEFUL

Ukisikia 'Another One' unaelewa Dj Khaled anachomaanisha right? June 16 ameachia chupa lingine kali akiwa na Kipenzi cha wengi, mwanadada Riri Rihanna na RNB Singer Bryson Tiller kwenye ngoma yake mpya Wild Thoughts.

Wild thoughts ni ngoma ya 4 kuachiliwa na Dj Khaled baada ya Shining, i am the one na To the Max.

Ni ngoma ambayo imesample nyuzi za ngoma ya 'Maria Maria' Product G&B, Carlos Santana

So far imeishafikisha views 15M (Millioni 15)  YouTube kwenye DjKhaledVEVO.

Dj Khaled ameachia ngoma hiyo ambayo itakuwepo kwenye album yake ya GRATEFUL itakayochomoka tarehe 23 June 2017.