Baada Ya Mapacha Huu Ndio Utakua Ujio Wa Beyonce

 

Kujifungua watoto mapacha hakujamfanya Beyonce ashindwe Kuwa mbunifu siku za hivi karibuni, Chanzo cha karibu na Familia ya "The Carter" kimeiambia HollyWoodLife Kuwa ujio wa mapacha hao umekua ukimshawishi Malkia Bey kuandika ngoma nyingi zaidi zitakazoingizwa kwenye Albamu yake inayoweza kuachiwa mwaka 2018.

"Mapacha na Blue Ivy wanamfanya Beyonce Kuwa na furaha ambayo hajawahi kuonekana nayo na amewekeza hisia zake zote kwenye muziki. Kwenye Albamu mpya ya Beyonce  kutakua na nyimbo kuhusu watoto wake na kizuri zaidi Albamu itawasili mapema April 2018" Kilisema chanzo hicho.

Hizi ni habari njema kwa mashabiki wa Beyonce kusikia kama malikia wao atakua anaamsha Dude jingine baada ya #Lemonade ambayo wikiendi iliyopita  ilifanikiwa kuchukua Tuzo ya #BET kama Albamu bora ya mwaka 2016/2017.

Nyumba Ya Milioni 894 Ambayo Beyonce Na JAY-Z Wamepanga Kwa Ajili Ya Mapacha Wao: