Baada Ya Lava Lava Huyu Ndiye Msanii Mpya Wa WCB?


Diamond Platnumz ameendelea kufungua mianya ya kusaidia vipaji vya dhati kabisa kupitia Record Label yake WCB ambayo mpaka sasa ina jumla ya wanamuziki 6 ambao ni mwenyewe Diamond Platnumz,Harmonize,Rayvanny,Rich Mavoko na Queen Darleen. Ujio wa  Lava Lava ambae alitambulishwa mapema mwezi huu unaweza kuwa ni neema kwa rapa kutoka rapa Motra The Future.
 Akizitambulisha ngoma zake mbili kwenye XXL ya Clouds FM, Diamond Platnumz alipata fursa ya kusikiliza hitaji la Mkali huyo wa Sina Koloni la kusaidiwa kufika mbali kimuziki. Baada ya kujiridhisha Diamond Platnumz na uongozi wake walikubaliana kumkalibisha Rapa huyo ofisi za WCB:

FULL INTERVIEW IKO HAPA"