Baada Ya J.A.F.F.E.R.Y Young Thug Amedondosha Beautiful Thugger Girls

Mwezi mmoja baada ya rapa Young Thug kuahidi ujio wa Albamu yake mpya ambayo rapa Drake amehusika kama Executive Producer.

Baada ya kuipa promo ya kutosha kwenye mitandao ya Instagram na twitter hatimaye Thugger amedondosha mzigo wake siku ya Jana.
Albamu hiyo ambayo mwanzo ilikua iitwe "Easy Breezy Beautiful Thuggee Girls" imetambulishwa Juni 16 kama "Beautiful  Thugger Girls"

Kwenye Beautiful Thugger Girls Young Thug amewaunganisha Millie,Lil Dirk, Jacquees, Future & Snoop Dogg. Jumla ya ngoma 14 zinapatikana kwenye Albamu hiyo.