Anto Neosoul amtaja Msanii wa Bongo anayekiki zaidi Kenya kwa sasa.


Anto Neosoul ni moja ya msanii kutoka Nairobi Kenya ambaye alikuja Bongo kurekodi ngoma na Producer kutoka The Industry Nahreel.

Mchongo huo umefanyika bongo baada ya jamaa kukutana Nairobi wakati Nahreel yupo kule na kupeana contact.

Kupitia interview aliyofanya Anto Neosoul kwenye The Playlist Times FM, June 17 baada ya kuulizwa ni wasanii gani ambao wanafanya poa saivi kule kwao Kenya? Anto Neosoul alimtaja Rayvanny kama msanii kutoka TZ anayetrend sana sasa hivi.

Rayvanny so far amefanya collabo na Khaligraph kwenye chalii ya ghetto, Bahati - Nikumbushe na yupo kwenye msimu wa 5 wa Coke Studio Afrika ambao unafanyika nchini Kenya na aliweza kukutana na msanii mkali kutoka Marekani Jason Derulo na wengine kibao kutoka Afrika.

Pia ni msanii pekee kutoka Afrika Mashariki aliyependekezwa kwenye tuzo za BET kwenye category ya Best New International Viewers Choice Award 2017. 

mpigie kura hapa, bonyeza link hii  http://www.bet.com/shows/bet-awards/2017/bet-international/nominees/international-viewers-choice-award.html


TAZAMA FULL INTERVIEW YA ANTO NEOSOUL Hapa: