Vitu Vitatu Ambavyo T.I Ameahidi Kufanya Kabla Ya Kustaafu.


Tangu mwaka 2012 Mwanamuziki T.I amekua akiongelea kuhusu kuachana na muziki wa Rap Kwa mujibu wa AllhiphopNews inaonekana T.I yupo kuupiga chini muziki wa Rap. Mapema mwaka huu kwenye moja ya mahojiano yake na The Breakfast Club T.I alikaliliwa akisema amepanga kurekodi albamu tatu za mwisho na baada ya hapo kiroho safi hatotambulika kama Rapa.Star huyo wa ngoma kama "No Mediocore", "Live Your Life", "Whatever You Like" na nyingine nyingi anatajwa kuwa na umiliki halali wa albamu tisa kwa kipindi chote cha muziki wake, mnyamwezi hakusita kuzitaja kwa majina albamu hizo akisema Albamu yake ya 10 itaitwa "Trap Music" ya 11 itaitwa "Dope Boy Meets Girl" huku akimaliza na "Kill The King" baada ya hapo usitegemee kumsikia kwenye Rap tena. Kupitia Interviews na mikutano kadhaa anayofanya T.I amekua akiepuka maswali mengi likiwemo la kipi atafanya baada ya kuachana na rap, Lakini inasemekana tayari ameshalamba dili kadhaa za kuonekana kwenye Movie na TV SHOWS kadhaa.   Kwa sasa ngoma Latest ya T.I ni "I Believe" ambayo inapatikana kwenye plattforms zote za muziki na mitandao mbalimbali.

CHEKI NAYO HAPA: